22 Julai 2025 - 14:06
Kukamatwa kwa Mawakala 87 wa Utawala wa Kizayuni katika Mkoa wa Lorestan, Magharibi mwa Iran

Watu hao 87 waliotiwa mbaroni wanatuhumiwa kwa kueneza hofu miongoni mwa raia, kufanya vitendo vya uharibifu, kuwasiliana na mashirika ya kijasusi ya kigeni, na kumiliki vilipuzi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lorestan (Magharibi mwa Iran) ametangaza kukamatwa kwa watu 87 waliokuwa wakishirikiana na utawala wa Kizayuni katika eneo hilo na kuwasilishwa kwa vyombo vya Sheria.

Brigedia Yahya Elahi, siku ya Ijumaa alisema: “Wakati wa vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni, Polisi wa Mkoa wa Lorestan waliweza, kwa msaada wa taarifa za kijasusi, ushirikiano mzuri, na uungwaji mkono wa Wananchi, kuwatia mbaroni watu 87 waliotuhumiwa kwa kueneza hofu miongoni mwa raia, kufanya vitendo vya uharibifu, kuwasiliana na mashirika ya kijasusi ya kigeni, na kumiliki vilipuzi.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha